Accessories zimeongezea utam zaidi |
Apple's Kitchen Party - Makeup,Accessories & Hair "Bianca Salon"
APPLE ndio jina la bibi Harusi huyu, ni Classmate wangu, na mdogo wangu wa chuo, nimefurahi sana kumkuta leo Salon na kumpamba, ye mwenyewe hakujua kama atanikuta na hakuamini kilichotokea baada ya hapo....Amefurahia sana kazi zetu, hakuna kitu kizuri kama mteja kuridhika na kupenda kazi yako, Muangalie alivyo Mzuri Mshalaah mtoto wa Kiislam Jicho nyanya, her smile... Cute wewe!! Ilikua ni Kitchen Party yake na Tunamtakia kila la kheri.
**Mac cosmetics£Smokey eyes£Orange lipstick 'Sephora'**
Preg. in style
Nani Kasema ukiwa Mjamzito usijipende wala kupendeza?? Fashion zipo kibaoooo, kuanzia nywele, Tops, Pants, dresses, skirts, shoes, and nails tukija kwenye makeup ndo kabisaaa.... Sijakwambia ukachague nguo isiyokutosha!! Kisa umeenda na Fashion lahasha, tena mwanangu usimbane kabsaa, vaa nguo yenye lastik ikiachia mtoto apumue na kukufanya wewe kuwa comfortable... Sio unavaa nguo ukiingia sehem kila mtu anajiuliza huyu nae vipi? Mimba imemuijia vibaya eeeeh??? lol, Mi nawakubali sanaa, napenda kuona tuwasafi all the time...
Kwetu Pazuri
Made in Tanzania, Kiki mmenigusa Plus size, Mchanganyiko wa rangi na mishono imenogaje sasa? tujivunie na kazi za mikono yetu.... Good Job!!
Urembo Asilia - Avocado & Honey Mask for Dry Skin
Kidokezo cha leo:-
Avocado
and Honey Mask for Dry Skin (Mask ya Parachichi na Asali, kwa ngozi Kavu)
Hii face mask ni nzuri sana kwa wale ambao
wana ngozi kavu saana. Inasaidia kulainisha, (moisture).
Mahitaji:
- Parachichi (lilioiva) nusu kipande
- ¼ au ½ kikombe cha asali
- Kijiko 1 kikubwa olive oil
- Maji ya limau 1
Kwenye chombo, changanya vitu vyote pamoja.
Osha uso wako vizuri na sabuni yako ya kila
siku, jifute vizuri.
Paka mask kwenye uso hadi shingoni, acha
kwa dakika 10 hadi 15 usizidishe mda.
Baada ya hapo osha uso na shingo na maji ya
uvuguvugu na kausha. Kisha pakaa mafuta yako ya kila siku au ya nazi au olive
oil pia ni mazuri.
Hii mask ni nzuri kwa nywele pia za natural
hata zenye dawa. Unapaka baada ya kuosha nywele, unaweka mask kwenye nywele acha
kwa dakika 15 hadi 20, osha na shampoo vizuri, kausha na style.
Kumbuka, hata kama vitu vyote hivi ni vya
asilia (natural), tunakushauri kuepuka kupatwa na allergy, fanya test ya hii
mask, kwenye mkono au mguu, paka acha kama dakika 10 hadi 15, uone kwanza. Hii ni kwa sababu kuna watu wana allergy na
vitu asilia pia.
ENJOY UR WEEKEND!!
Labels:
Bridal Care
Subscribe to:
Posts (Atom)