From the Runway: Eye Shadow za Tattoo

Eye Shadow za Tattoo: Yes au No?
Mimi naona kama ni kwenye Photo shoots na Fashion Shows YES. Ila kwa mtoko? Kazi kwetu.



KWETU PAZURI - Mishono

Ukizingatia hii ni miezi ya mashughuli basi usipate shida tutakuwekea mishono ya kila aina, ili mradi tu ushaini... Wa ukweli mpo??









UREMBO ASILIA: Turmeric & Yoghurt Facial Mask (Mask ya Manjano na Mtindi)









Kidokezo cha leo:  Turmeric and Yoghurt Facial Mask (Mask ya Manjano na Mtindi)

Hii facial imetokea Bara la Asia, nchi ya India. Hutumiwa saana na mabiharusi, zile wiki chache kabla ya harusi. Inasaidia kusafisha ngozi na kuifanya iwe laini, pamoja na kupunguza madoa na chunusi usoni. 

  • Unga wa Dengu kijiko 1 kibukwa
  • Manjano kijiko kimoja na nusu cha chai
  • Mtindi mweupe (plain yoghurt)
Kwenye chombo, changanya vitu vyote pamoja.
Paka mchanganyiko kwenye uso hadi shingoni, acha kwa dakika 15 hadi ikauke.
Baada ya hapo osha uso na shingo na maji ya uvuguvugu na kausha. Kisha pakaa mafuta yako ya kila siku au ya nazi au olive oil pia ni mazuri. 

* Usihofu uso wako hautakuwa wa njano, bali utakuwa na rangi nzuri na ya kuvutia*

Kumbuka, hata kama vitu vyote hivi ni vya asilia (natural), tunakushauri kuepuka kupatwa na allergy, fanya test ya hii scrub, kwenye mkono au mguu, paka acha kama dakika 15 hadi 20, uone kwanza.  Hii ni kwa sababu kuna watu wana allergy na vitu asilia pia.
 

Una Maswali mengi kwani we ni POLISI??

Mtu katoka nyumbani kwenye kioo kajiangalia, na bado yuko na bado Baby wake kamuhakikishia kuwa HAKUNAGA.... we unauliza hiyo mbona kama Brazia? Katokaje ndani?? haya mavazi gani sasa??? Huyu siku izi ana data nini??? Iga ufe.... na ukiiga angalia shepu baby... Tumbo? Ziwa? Kifua? Mikono? Mabega? Hips??






Kwetu Pazuri - Handbags







Mr & Mrs Mark Oppong - Makeup, Hair & Bouquet by Bianca Salon

































Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...