Kucha...kucha...kucha....











Mwanamke kucha, hii nimeileta maalum kwa ajili yetu sisi, ningependa kuengelea yafuatayo:

Maharusi:- Kutokana na experience yangu ya kupamba maharusi huwa tunawashauri wapake rangi zilizopoa ambazo sio kali haswa siku ya harusi... kiukweli hautapendeza kama umepaka crazy colors siku ya harusi yako ila kama umependa hautakatazwa, mara nyingi huwa fashion ile inapoisha na wewe una picha za kumbukumbu nyumbani ndio unaanza kujutia

Wanawake Maofisini:- Kwa mara yako ya kwanza kabisa unaenda kufanya interview unatakiwa kuwa very smart ikiwemo kucha zako kuwa safi na rangi kama zilizoko hapo juu, unaingiaje kuomba kazi tena kwenye jopo la watu wenye rika na makabila tofauti tofauti mkono  una mdogo wa kuku au miguu ya bata? rangi ulizopaka kama rainbow, hapo ndugu hata kama una qualify... watu wameshakushusha thamani na lazima watajiuliza huyu leo inteview kaja hivi je akianza kazi si ndio balaaa??? Sasa ukute ndo huna hizo qualifications weeeee...

Mwanamke nyumbani:- Haimaanishi eti ukiwa ni mama wanyumbani, baba, au dada basi kucha zako ziwe ndo chafu, kumbuka usafi unaanzia nyumbani unavyokuza familia yako kwa kucha chafu basi watoto watarithi maradhi hayo... Kumbuka mtoto uleavyo ndivyo akuavyo...

Wanafunzi:- Hii haina mjadala mwanafunzi kufuga kucha na kuzitreat kikubwa haipendezi, tena inakupotezea muda wa masomo, kucha zikiwa safi na fupi zinapendeza zaidi.

Kifashionista zaidi:- Inaeleweka fashion za kucha zinakuja kila mara ila unatakiwa kuzingatia ukowapi na unakutana na watu wa aina gani


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...