Bianca Salon Blog: Inakuletea kipengele kipya cha vidokezo, maoni na njia totafuti za kutengeneza na kutumia vitu, mafuta, vyakula etc vya aina tofauti kwa ajili ya uso, mwili na nywele.
Kidokezo cha leo: Cucumber and Honey under Eye Mask
(Matango
na Asali, kupunguza weusi wa chini ya macho)
- Tango 1
- Asali (Kijiko 1 kikubwa)
- Unga wa dengu/Unga Mahindi (kijiko 1 kidogo) (ili mask iwe na kauzito kidogo)
Weka kwenye chombo, kwaruza
tango, kisha weka asali na unga wa dengu/mahindi.
Changanya pamoja vizuri, uso ukiwa msafi na mkavu, paka
chini ya macho au pahala popote usoni penye weusi, acha kwa dakika 15 hadi 30,
futa na kitambaa cha uvuguvugu au osha uso na maji kisha paka
mafuta/moisturizer yako uitumiayo kila siku au Olive oil ni nzuri zaidi.
Hata kama vitu vyote hivi ni
natural. Tunakushauri kuepuka kupatwa na allergy, fanya test ya hii mask kwenye
Mkono au mguu, paka acha kama dakika 15 hadi 30, uone kwanza. Hii ni kwa sababu kuna watu wana allergy na
vitu asilia pia.
""Asanteni sana till next time.... Usikose kuna mambo mazuri zaidi na zaidi yatakuijia hapa hapa"" Jipende