Leg and foot scrub after Waxing (Scrub ya
Miguu na unyayo baada ya Wax)
Kwa wale wanao wax miguu au hata mikono,
hii scrub ni nzuri kupaka baada ya wax. Inasaidia kufanya ngozi kuwa laini na
relax ngozi baada ya moto wa wax.
Mahitaji:
- Machicha ya nazi ½ kikombe
- Sukari ya brown ¼ kikombe
- Limau au ndimu vijiko Vidogo 3
- Kijoko 1 kikubwa coconut oil au almond oil
Kwenye kibakuli changanya kila kitu pamoja.
Baada ya wax au shave paka scrub kwenye
miguu hadi unyayo na sugua vizuri kwa dakika 5 hadi 10. Baada osha na sabuni
yako ya kila siku. Halafu paka mafuta ya nazi, olive au yoyote.