Kidokezo cha leo: Turmeric and Yoghurt
Facial Mask (Mask ya Manjano na Mtindi)
Hii facial imetokea Bara la Asia, nchi ya India. Hutumiwa
saana na mabiharusi, zile wiki chache kabla ya harusi. Inasaidia kusafisha
ngozi na kuifanya iwe laini, pamoja na kupunguza madoa na chunusi usoni.
- Unga wa Dengu kijiko 1 kibukwa
- Manjano kijiko kimoja na nusu cha chai
- Mtindi mweupe (plain yoghurt)
Kwenye chombo, changanya vitu vyote pamoja.
Paka mchanganyiko kwenye uso hadi shingoni, acha kwa dakika 15 hadi
ikauke.
Baada ya hapo osha uso na shingo na maji ya uvuguvugu na
kausha. Kisha pakaa mafuta yako ya kila siku au ya nazi au olive oil pia ni
mazuri.
* Usihofu uso wako hautakuwa wa njano, bali utakuwa na rangi nzuri na ya kuvutia*
Kumbuka, hata kama vitu vyote hivi ni vya asilia (natural),
tunakushauri kuepuka kupatwa na allergy, fanya test ya hii scrub, kwenye mkono
au mguu, paka acha kama dakika 15 hadi 20, uone kwanza. Hii ni kwa sababu kuna watu wana allergy na
vitu asilia pia.